Luke 2:25-30

25 aBasi alikuwako huko Yerusalemu mtu mmoja jina lake Simeoni, ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu, akitarajia faraja ya Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 bRoho Mtakatifu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Al-Masihi wa Bwana. 27 cSimeoni, akiwa ameongozwa na Roho Mtakatifu, alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Isa ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Sheria, 28ndipo Simeoni akampokea mtoto mikononi mwake na kumsifu Mungu, akisema:
29 d“Bwana Mwenyezi, kama ulivyoahidi,
sasa wamruhusu mtumishi wako
aende zake kwa amani.
30 eKwa maana macho yangu yameuona wokovu wako,
Copyright information for SwhKC